Kuhusu hili kanisa jipya lililofunguliwa Kigoma linalokataza watu kwenda hospitali.

Licha ya serikali kulipiga marufuku
dhehebu lililoibuka katika kijiji cha
Rumashi wilaya ya Kakonko mkoani
Kigoma liitwalo Sabato matengenezo,
mwanzilishi wa dhehebu hilo amejitokeza
na kusisitiza kuendelea na imani hiyo.

Baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa
dhehebu hili ambalo linakataza watoto
kwenda shule na wagonjwa kutibiwa
hospitalini, Serikali ilimkamata kiongozi
wake pamoja na waumini kadhaa lakini
baadae wakaachiwa huru.

Alieanzisha hili dhebebu anaitwa
MEDADI LAURENT ambae baada ya
kukamatwa alihukumiwa kifungo cha
miezi miwili jela au faini ya shilingi
30,000/.

Anasema ‘kama ni baridi unapaswa uwe
baridi, kama ni moto unapaswa uwe
moto, kama nilivyosema toka mwanzo
mimi mpaka dakika ya kufa sina mpango
wa kusomesha mtoto isipokua kile serikali
itachoamua ndio ifanye’
Mmoja wa waumini wa kike wa kanisa hili
Amesema kwamba ‘sisi
elimu tunayoijua ni elimu ya kumfahamu
mtakatifu alie juu maana ndipo kuna
uzima lakini katika elimu ya dunia hakuna
uzima, maana tunawashuhudia wasomi
wengi wakifa hawapati uzima lakini sisi
hata tusiposoma elimu ya dunia hii kama
tutamtii Mungu au hata kama tutakufa
tutakua na uzima wa baadae’
Muumini mwingine wa kiume ‘swala la elimu siafikiani
nalo kwa sababu kwanza kwa mujibu wa
maandiko matakatifu hatupaswi kujifunza
elimu nyingine tofauti na elimu ya
kumjua Mungu maana ukisoma Yohana
anasema na uzima wa milele ndio huu
wakujue wewe Mungu wa pekee na Yesu
kristo uliemtuma.

Mkuu wa wilaya ya Kakonko Peter Toyima
amesema ‘tumeandika barua kuliandikia
lile dhehebu kwamba ni marufuku
kuendelea na shughuli hizi kwa sababu
kwanza hawajasajiliwa kwa hiyo hamna
uhalali wa kuwepo na wakifanya tena
mkusanyiko wa namna hiyo lazima
tuwakamate na hatua zichukuliwe tena.

Dhehebu la Sabato Matengenezo
lilianzishwa January 2014 baada ya
kujitenga kutoka katika dhehebu la
Waadventista wasabato.

No comments

Theme images by jangeltun. Powered by Blogger.