Rais Mpya wa Malawi ana Msimamo Mkali Ziwa Nyasa, Asema Haya
Wingu jeusi limeanza kutanda kuhusu hatima
ya mzozo wa Ziwa Nyasa kutokana na
msimamo wa hivi karibuni wa kiongozi wa
Democratic Progressive Party (DPP), Peter
Mutharika ambaye sasa ni Rais mpya wa
Malawi.
Hiyo inatokana na msimamo wa Mutharika
ambaye ni Profesa wa Sheria wa kupinga
kuendelea kujadiliana na Tanzania kuhusu nani
mwenye haki ya kumiliki ziwa hilo alioutoa
wakati alipowatembelea wananchi wa Chipoko,
kando ya ziwa hilo miezi michache kabla ya
uchaguzi mkuu ambao ulimwigiza madarakani.
Pamoja na kwamba mazingira ya msimamo huo
yanaweza kutofautiana na hali halisi ya sasa,
tofauti za kisiasa baina yake na mtangulizi
wake, Joyce Banda zinaweza kuongeza
msukumo mpya wa kutaka kutoendelea na
mazungumzo ya mpaka wa ziwa hilo.
Akizungumza na wananchi hao, Profesa
Mutharika aliwatoa wasiwasi na kuwataka
kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa
maelezo kuwa ziwa hilo lipo kwenye himaya ya
Malawi na kwamba kuendelea kujadiliana na
Tanzania ni kupoteza muda.
“Hakuna haja ya kuendelea kujadiliana, Ziwa
Malawi ni mali ya Malawi na litaendelea kuwa
la Malawi daima,” alisema Mutharika ambaye
pia amewahi kufundisha sheria Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.
Alimshutumu Banda na kudai alikuwa dhaifu
kiasi cha kutoa fursa kwa Tanzania kutumia
udhaifu huo kutaka kupora ziwa hilo.
“Ziwa hili letu ila Tanzania inatumia tu udhaifu
wa Serikali iliyopo kwani wenyewe wanajua
ndani ya mioyo yao kuwa hawana chochote
katika ziwa hilo. Tutakaporejea serikalini
mwakani haya mambo yote yasiyo na kichwa
tutayamaliza. Nataka niwahakikishie kwamba
tutapeleka meli zaidi kwenye ziwa hili ili kuinua
shughuli zetu za kiuchumi na kutengeneza ajira
kwa vijana wetu.”
Hata hivyo, wiki iliyopita Serikali ya Tanzania
ilitoa msimamo wake kuhusu mzozo huo wa
mpaka na kudaia kuwa itaendelea kujadiliana
na Malawi.
Akizungumza bungeni wakati akiwasilisha Bajeti
ya wizara yake, Waziri wa Mambo ya nchi za
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe alisema Tanzania ilikuwa ikifuatilia kwa
karibu uchaguzi wa Malawi na kwamba iko
tayari kufanya kazi na serikali yoyote
itakayoingia madarakani.
No comments