Hii ndio mbinu inayotumiwa na Matajiri wa Urusi kukwepa foleni town
Sote tunafahamu kwamba Ambulance ni
magari yanayotumika kubeba na kuwaisha
wagonjwa kutoka sehemu fulani kwenda
sehemu nyingine na uwapo barabarani kama
dereva ni lazima upishe Ambulance inayopita
ili iokoe maisha ya mgonjwa ila matumizi ya
Ambulance huko Urusi sio ya Wagonjwa peke
yake.
Unaambiwa moja ya tabia za matajiri wa
Urusi ni kukodi magari feki ya wagonjwa
(Ambulance) ili kukwepa foleni hasa kwenye
jiji la Moscow ambalo lipo kwenye list ya majiji
yenye foleni kubwa sana duniani ambapo
matajiri hao hulipia safari moja kwa zaidi ya
shilingi laki tatu za kibongo.
Ambulance hizi feki zinatofautiana na zile za
hospitali kwa ndani lakini kwa nje ni kama
Ambulance ya kweli ambapo hizi feki ndani
yake kunapatikana huduma kama za TV,
vinywaji vya aina mbalimbali, hata makochi
yametengenezwa vizuri sana ambapo uzuri
huo unafananishwa na magari ya kifahari ya
Limousine na wakati mwingine kwenye hizi
ambulance kunakua na Wanawake maalum
ndani yake kwa ajili ya kutoa kampan kwa
mteja.
Rais Putin na Waziri wake mkuu huwa
wanapita na msafara huku magari yao yakiwa
yana taa maalum za blue ambazo ni ishara
kwa kila mmoja kwamba msafara wa kiongozi
mkuu uko barabarani.
Polisi wamekua wakijaribu kuzisimamisha
lakini sio zoezi ambalo lina mafanikio.
No comments