Saa chache baada ya hotuba ya Rais Kikwete,hiki ndicho walichokisema vyama vya upinzani.

Wenyeviti wa vyama vya Upinzani kutoka
Chadema,Chama cha Wananchi (CUF) na
Chama cha NCCR-Mageuzi, jana usiku March
21 mara baada ya hotuba ya Rais March
walikutana ili kutoa kauli ya pamoja kutokana
na hotuba ya ufunguzi wa Bunge kwa
maelezo kuwa tayari Rais amevuruga
mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya.
Wakati viongozi hao wakikutana Mwenyekiti
wa Chama cha DP Mchungaji,Christopher
Mtikila alisema Rais ameingilia mchakato na
kutoa maelezo jinsi ya kuandika Katiba.
Wakizungumza mara baada ya hotuba hiyo
Mwenyekiti wa Chadema Freeman
Mbowe,James Mbatia na Profesa Ibrahim
Lipumba,walisema wameipokea kwa
masikitiko makubwa hotuba hiyo.
“Tunakwenda kujadili hotuba ya Rais na
tutatoa msimamo wetu,” alisema Mbowe.
Awali Katibu wa muda wa Umoja wa Katiba
ya Wananchi (Ukawa),Julius Mtatiro alisema
Rais Jakaya Kikwete amevuruga mchakato wa
Katiba, kwani walitarajia angetumia mamlaka
yake kama Rais kuwaunganisha.
“Rais tulitarajia angeongea kama mkuu wa
nchi, lakini amezungumza kama Mwenyekiti
wa CCM na kutoa msimamo juu ya muundo
wa Muungano jambo ambalo
hatukulitegemea,” alisema Mtatiro.
Alisema kwa Rais kutoa msimamo ni sawa na
mwongozo jambo ambalo limevuruga
mchakato mzima.

No comments

Theme images by jangeltun. Powered by Blogger.