KWANINI MAMBO HUWAENDEA MRAMA WASANII WANAO JITOA TIP-TOP CONNECTIONS
Wako wapi MB Dog, Z-Anto, Keisha, Pingu,
Spark, Dongo Janja na wengine waliowahi
kujitoa Tip Top Connection? Kuna nini Tip Top,
kwamba ukijiondoa tu huwezi kufanikiwa
mbeleni? Kwanini ni wasanii wachache tu, tena
anaweza kuwa Cassim Mganga peke yake
ambaye baada ya kujiondoa kwenye himaya
hiyo yenye makazi yake Manzese jijini Dar es
Salaam, amefanikiwa kuwa na career ya
kueleweka? Wengine wote, wamefeli.. big time.
Kinachosikitisha zaidi ni kuwa wengi
wakiondoka hutoa maneno ya kashfa na hivyo
kujikuta wakinyea kambi.
Hebu tuwaangalia hawa watatu, Dogo Janja, Z-
Anto na MB Dog
Dogo Janja
Unakumbuka June 2012, kipindi Dogo Janja
ameondoka Tip Top? Habari hiyo ilikuwa kubwa
kiasi ambacho simu za Madee na Dogo Janja
zilikuwa busy kwa interview. Kila pande ilikuwa
ikiutupia lawama upande wa pili.
Kama umesahau wacha tukukumbushe
ilivyokuwa.
Sababu zilizotajwa na Tip Top Connection ni
kwamba Dogo Janja alilewa sifa na kuwa mtoro
shuleni.
Kwa mujibu wa interview aliyofanya na Bongo5,
uonevu na dhuluma ndivyo vilivyomchosha
Dogo Janja kuishi Dar es Salaam na kujiondoa
kwenye himaya hiyo.
Alisema tangu aje Dar es Salaam hakuwahi
kusaidiwa chochote na Madee zaidi ya mambo
ya muziki pekee huku kula, malazi na ada ya
shule vikifanywa na rafiki yake Madee aitwaye
Abdallah Doka ambaye (Dogo Janja) alikuwa
akiishi kwake.
Alisema kutokana na ngoma zake kujipatia
umaarufu alikuwa akipata show nyingi nchini
na zote alikuwa halipwi chini ya milioni moja.
Kilichokuwa kinamsikitisha anasema ni kulipwa
hela kidogo isiyozidi laki mbili na hivyo
kumfanya aishi kwa tabu licha ya kuingiza hela
nyingi za show. “Nilikuwa navumilia tu bro
kwasababu kila nilipolalamika kuhusu mambo
ya hela Madee alikuwa mkali sana,” aliiambia
Bongo5.
Dogo alidai ilikuwa inafikia wakati akifanya
show za ukumbuni hulipwa elfu hamsini au
chini ya hapo na wakati mwingine alikuwa
halipwi kabisa. Alisema tamaa ilizidi kumwingia
Madee kiasi cha kumnyang’anya kadi yake ya
benki na kuanza kuchukua hela bila kujua
password aliipata wapi. “Kuna wakati nilikuwa
nataka kumtumia mama laki moja, Madee
akanikataza eti kwakuwa watadhani nina hela
sana,” alisema.
Aliongeza kuwa kuna siku Madee alimpigia simu
na kumwambia kuwa kaka yake wa Kibaha
ameandaa show ya CCM na angemlipa shilingi
laki moja. “Hivi kweli bro mimi ni mtu wa
kufanya show ya laki moja?” alihoji. Hata hivyo
aliamua kukubali ili kuepusha lawama.
Baada ya show kumalizika alisema yeye na
back up artist wake walirudishwa saa saba
usiku wakati asubuhi yake alitakiwa kwenda
shuleni kuchukua namba ya mtihani na
kuandaa dawati la kukalia. Dogo Janja alisema
kuwa ilimuuma sana kwakuwa muziki haujampa
chochote licha ya Madee ambaye huwa hapati
hata show kumtumia kimaslahi na hadi kufikia
hatua ya kujenga nyumba yake.
“Ni kama vile Madee alinipanda ili anivune,”
alisema.
Alifunguka kuwa hadi kufikia Tip Top watangaze
kumfukuza alikuwa kwa Tundaman akipiga
story na Madee akamuita kisha kuanza
kumpiga na kwamba alichukua simu yake
akaondoka nayo. “Jamaa alianza kujitumia
meseji kutoka kwenye simu yangu kwenda
kwake za matusi ama kuwa nataka kumroga.
Jana nimemuonesha Milard hizo meseji na
amesikitika sana.”
Alisema kitendo cha kumwambia Madee kuwa
amechoka na anataka kurudi nyumbani ndicho
kilimfanya amfanyie yote hayo hadi
kumwambia kuwa watahakikisha wanambania
asifanye vizuri tena kwenye muziki. Pia amedai
kuwa Madee aliwapigia simu wazazi wake ili
wamkataze Dogo Janja asifanye interview na
vyombo vya habari.
“Wanajua nikiongea wataabika sana.”
Baada ya drama zote hizo ndipo Ostaz Juma
akaingia kwenye picha. Alimtumia nauli ya
ndege rapper huyo kutoka Arusha kurejea Dar
na akajiunga na Mtanashati Entertainment
ambayo wakati huo ilikuwa na heshima kidogo.
Dogo Janja alipewa maisha, akalipiwa ada ya
shule na kutoa ngoma iitwayo Ya Moyoni
aliyomshirikisha PNC. Haikupita muda, mambo
yakaanza kutokota.
Kwa mara nyingi Ostaz Juma alimfukuza na
kumrejesha tena rapper huyo kwa madai kuwa
hakuwa na nidhamu. Hata hivyo, imefika wakati
ambapo Mtanashati Entertainment imekosa
muelekeo na Dogo Janja anahisi meli inazama.
Kuomba msamaha ili mambo yaende ni kitu
kisichoepukika kwake kwakuwa ni kweli Dogo
Janja wa ‘Mtoto wa Uswazi’ ft Godzilla
amepotea kabisa.
Z-Anto
Ni ngumu kuamini ukubwa wa Z-Anto baada ya
kutoa hit single yake ‘Binti Kiziwi’ ungekuja
kuyeyuka kama barafu ikutanapo na jua kali.
Enzi Binti Kiziwi inahit, hakuna msanii
aliyekuwa na show nyingi kama Z-Anto. Hata
hivyo, meneja wa Tip Top Connection aliwahi
kudai kuwa kipindi hiki ndipo msanii huyo
alianza kuota ‘majipu’ kwapani na kuanza pozi
nyingi. Jambo hilo lilimkera Babu Tale kiasi cha
kuamua kuifuta kabisa video mpya ya msanii
huyo iliyokuwa inategemewa kumpeleka juu
zaidi. Baada ya kuondoka Tip Top mpaka leo
hii, Z-Anto si yule tena wa zamani na ukweli
hali yake kimuziki ni mbaya.
“Nililazimika kushuka kwa sababu hiyo. Lakini
nilipokuja kuzigundua zile njia nikaweza
kupenya na ngoma binafsi nilijisimamia
mwenyewe kwa kila kitu ambayo ndio hiyo
Kisiwa cha Malavidavi,” Z-Anto alikiambia
kipindi cha Mseto cha Radio Citizen ya Kenya
hivi karibuni japo alidai kuwa hadi leo Babu
Tale anamtaka arejee kundini.
“Mpaka kesho (Babu Tale) bado ananipenda.
Hata ukimuuliza katika wasanii wake
anaowapenda atatajwa wawili asishindwe
kunitaja mimi.”
MB Dogg
Unazikumbuza Latifa na Si Uliniambia? Hizo ni
miongoni mwa nyimbo bora za Bongo Flava za
muda wote lakini yuko wapi MB Dogg? Kama
ilivyokuwa kwa Z-Anto, naye baada ya kujitoa
Tip Top, mambo yalienda mrama. Ilimchukua
miaka mingi MB Dogg kuweka ‘ego’ pembeni na
kukubali kuwa kweli amepotea na anaiihitaji Tip
Top kiasi cha mwaka huu kuweka mambo sawa
na Babutale.
“Lakini kwa sasa nataka tumuangalie Mb Dogg
kwa macho mawili,” Tale aliiambia Millaayo.com
hivi karibuni. Mb Dogg ana kipaji watu
wanaujua uwezo wa Mb Dogg, Mb Dogg sio
kama amepotea hapana ila hana uongozi
anahitaji promo ya nguvu tu akipata hiyo
anarudi kupiga hela kama zamani.”
Hata yeye mwenyewe MB hivi karibuni alikiri
kuwa kufanya muziki bila kuwa na uongozi wa
kukusimamia ni kazi bure.
“Tip Top nilitoka na ndio kitu ambacho
kilinirudisha nyuma sana,” MB Dogg aliiambia
Bongo5 March 17 mwaka huu.
“Pale nilikuwa nafanyiwa kila kitu, nilikuwa
narekodi tu kazi yangu vitu vingine vyote
wanafanya wao so baada ya kutoka na
kujisimamia mwenyewe nikaanza kuyumba na
kuhangaika huku na kule. Kwahiyo kitu
ambacho nimegundua msanii bila management
nzuri huwezi fika mbali asikwambie mtu. Msanii
anahitaji kuongozwa, kushauriwa na mambo
mengine. Sasa hivi nipo Tip Top tumeingia
makubaliano mapya ya kazi ndio maana
nashukuru Mungu ngoma yetu mpya
‘Umenuna’ inasonga kidogo kidogo mpaka
kieleweke.”
Kinachowaumiza zaidi wasanii walioondoka Tip
Top ni kwamba wasanii waliosalia mathalani
Madee, wameendelea kufanikiwa zaidi. Mwaka
jana pekee, Madee anadai kuingiza zaidi ya
shilingi milioni 150 kwa single yake moja tu ‘Sio
Mimi’. Meneja wa Tip Top, Babu Tale
akishirikiana na Said Fela ndio walio nyuma ya
mafanikio ya Diamond Platnumz, kwahiyo ni
wazi kuwa Babu Tale ni ‘hot cake’ kwa sasa na
ndio maana wasanii wa Tip Top waliojiondoa
wako radhi kumuomba msamaha ili warejee
kundini.
Swali ninalokuacha nalo msomaji ni Je!
Haiwezekani msanii aliyejiondoa Tip Top kuwa
na career yenye mafanikio?
No comments