NDEGE YA MALAYSIA
Kama ndege ya Malasyia
ingepotea hapa Tanzania ingekua hivi:
Rais angehutubia taifa.bendera
zingepepea nusu mlingoti.
Kungekuwa na siku tatu za
maombolezo.Ingeundwa tume ya
kuchunguza. Ambayo ingelipwa
kila siku laki5.
Baada ya ndege kuacha
kuonekana ingeundwa tume
nyingine ya kuichunguza tume ya
kwanza.Lakini magazeti
yangeuzwa sana hasa gazeti la
Ijumaa.Kwanza lingeandika rubani
alikataa kurusha ndege
akalazimishwa. Baadae
lingeandika imeonekana Mtwara.
Gazeti la mwananchi lingeandika
abiria walikuwa 250 Majira
lingeandika abiria walikuwa
289.Nipashe lingeandika abiria
275.
Lakini CHADEMA nao
wangeandamana nchi nzima ili
Mwakyembe ajiuzulu.
Masoud kipanya angechora katuni
ya mtu kashika darubini anatafuta
ndege.
Wasanii wa bongo fleva
wangetunga wimbo wa
pamoja.Kama John Komba
angechelewa kutunga.
TBC1 wangekuwa na kipindi
maalum cha kuhusu hiyo ajali.
Pia zingechapishwa t-shirt
ambazo zingekuwa na picha ya
ndege. Zingeandikwa We will
always remember you.Magazeti
yangeuzwa kuliko yalivyouzwa
kwenye msiba wa baba wa
taifa.Lakini uchawi nao
ungehusishwa bila kusahau
freemasons.
No comments