MBOWE Mnatuhalibia Chama, Chadema Inazidi Kupoteza Mvuto

Mimi nasema tena kuwa mimi nimwanachama
hai wa CHADEMA, Nimemsema mh. Mbowe
kwakuwa yeye ndiye mwenyekiti wetu na mkuu
wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, haya
yanayoendelea kukishushia heshma chama
hayaoni? Dr. Slaa naye kama katibu wa chama
hayaoni?.
Ni aibu kubwa sana taasisi kubwa kama hii
yenye watu makini kiasi hiki kupambana na
mtu mmoja tena mwisho wake tunaishia
kupata aibu.
Kwani faida yetu sisi wananchi na wanachama
mkimmaliza Zitto Kabwe kisiasa ni ipi?
Hapo awali mmetengeneza migogoro wenyewe
kwa kumjengea tuhuma zisizo na ushahidi
kama taarifa kutoka makao makuu ya chama
kuhusu nyendo za ZZK toka mwaka 2008 kwa
kupokea pesa toka CCM, mbona hamjatuletea
ushahidi wa uhakika nasi tukajihakikishia?
Matokeo yake kila mmoja ameona utofauti wa
CHADEMA ya mwaka 2013 na CHADEMA ya
mwaka 2014.
Kwenye hili swala la leka dutigite, NSSFna
TANAPA mmefanya uchunguzi wa kutosha na
mkapata uhakika na mlichopeleka bungeni?
Tunataka ushahidi hapa ili na wananchi
tujihakikishie sio mnatuletea propaganda za
kijinga hapa na kuanza kuaminisha watu.
Nimesoma ufafanuzi wa Zitto mwenyewe, NSSF
na TANAPA nimesikitika sana kuona kuwa
maelezo haya kama ni ya kweli basi CHADEMA
ndio itazidi kupoteza mvuto.
Nashindwa kuwaelewa na hawa washabiki
wanaoshinda humu wakishabikia ujinga bila
hata kufikiri ilimradi Mbowe kasema.
Watu wanabaki kuchangia changia ujinga wao
humu hata katika ujenzi wa chama
hawaonekani wakidhani ndio ukomavu wa
chama kumbe ndio wanazidi kukibomoa chama.
Mnajifanya wanachama wa CHADEMMA kwa
kutetea hata ujinga wa baadhi ya viongozi ndio
mnazidi kukimaliza chama, mfano huyu huyu
ZZK alipoongelea kidogo habari za Mbowe
wengi wenu mlianza kulalamika kwanini
aongelee habari za Mbowe.
Sasa ZZK sio binadamu kama alivyo Mbowe au
kiongozi mwingine anayeweza kuumia
anapozushiwa na kuchonganishwa kwa
wananchi?
Mashabiki nawashauri acheni kupumbazwa.

No comments

Theme images by jangeltun. Powered by Blogger.